- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kusherehekea siku ya wanawake Duniani wilayani Manyoni wanawake wametakiwa kutambua kuwa wao wanajukumu kubwa sana katika Taifa hili katika kutimiza wajibu wao kusimamia haki zao pamoja na makuzi ya watoto na kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati akihutubia katika sherehe za maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kata ya saranda wilayani Manyoni
Mwagisa amesema kuwa kila ifikapo march 8 duniani kote wanaadhimisha siku ya wanawake lengo ikiwa ni kuweza kuwakumbusha wanawake majukumu yao katika malezi na makuzi ya watoto lakini pia kuikumbusha jamiikutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii , kuwasaidia wanawake kuweza kutambua haki zao na za watoto ambapo amewataka wanawake kuacha kusherehekea siku hiyo kwa mazoea bali wasimamie kauli mbiu na kuhakikisha wanaitekeleza na kuifanyia kazi kwa kutimiza majukumu yao.
Mwagisa aliongeza kuwa wajibu wa kila mwanamke ni kulinda haki na usawa kwa watoto na wanawake, nakuwataka wanawake kujua kuwa jukumu kubwa la kulea watoto ni la wanawake hivyo amewataka kuacha kujisahu kutimiza majukumu yao na badala yake wajitambue na kujua kuwa mtoto yeyote anapoharibikiwa mzigo huwa kwa mama yake
“mtoto mwenye hekima humfurahisha babaye bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamae maandiko yanasema pia, hivyo wanawake wenzangu tusijisahau tuhakikishe tunasimamia malezi ya watoto wetu huko majumbani na hata mitaani tujue kuwa mtoto wa mwenzio ni mtoto wako pia lakini ndugu zangu tusisherehekee tu kama mazoea bali tujue tunajukumu kubwa kama nguzo ya Taifa tusijisahau sisi wanawake, sambamba na kutia nguvu kauli mbiu yetu tuendelee kupambana na vitendo viovu vinavyojitokeza kwa wanawake na watoto”alisema Mwagisa
Mwagisa alipata fursa ya kuwapongeza walimu na kuwaomba waendelea kuwa chachu ya malezi na kupambana na vitendo viovu juu ya usimamizi na makuzi ya mtoto.
“kwa nini ninasema walimu, niaamini mnamchango mkubwa sana kama wanawake katika Taifa hili kwani nyie mnakaa na watoto wetu kwa masaa mengi hivyo ninaimani kuwa mnamchango mkubwa sana wa malezi zidi ya watoto wetu, niwaombe sana walimu tukumbushanena tusimamie malezi ya watoto wetu tutambuwe kuwa msichana wa leo ndiyo mwanamke wa kesho hivyo niwaombe sana tuwalinde mabinti zetu.”alisisitiza Mwagisa
Katika suala la maendeleo na kujikwamua kiuchumi Mwagisa aliwataka wanawake wa Wilaya ya Manyoni kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri lakini pia kushirikiana na ofisi ya Maendeleo ya jamii ya Wilaya kuweza kuibua vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato ili waweze kusimamia familia zao.
“ wanawake tukijikwamua kiuchumi tutaweza kusaidia wenza wetu kwani kwa kufanya hivyo tutapunguza kasi ya umaskini lakini pia itatujengea heshima tutaweza kujisimamia hivyo basi niwaombe tutumie mikopo mbalimbali na pia tufanyeshughuli mbalimbali ili tuweze kuleta tija ya maendeleo ya jamii yetu”aliongeza Mwagisa
Aidha Mwagisa amempongeza Mh Rais mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Manyoni amewaomba wamama kuweza kumuunga Mh Rais Samia Suluhu Hassan mkono katika kusimamia majukumu yote kama wanawake .
Awali akisoma taarifa ya maadhimisho hayo afisa maendeleo msaidizi Ostatila Mwilafi amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kumuuonyesha upendo ,mwanamke kutokana na mafanikio yake katika Nyanja mbalimbali kama vile siasa kijamii na kiuchumi, ni siku ambayo wanawake hutambuliwa kutokana namafanikio yao bila kujali mgawanyiko wa Taifa bila kujali kabila lugha itikadi utamaduni kiuchumi au kisiasa
Aidha amesema kuwa nchini Tanzania maadhimisho haya hufanyika ilikutathmini maendeleo ya mwanamke kuwakumbusha wadau na jamii kuhusu umuhimu wa wanawake katika kuchangia ujenzi wa Taifa aidha wanawake ni kitovu cha mabadiliko chanya katika jamii.
Mwilafi alisema Halmashauri ya Manyoni wanawake wamekuwa wakishirikishwa katika Ngazi zote hasa katika masuala ya kusimamia na kutekeleza mipango ya kimaendeleo aidha wanawake wamejengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yanayotolewa na wadau na Halmashauri pia wamewezeshwa kiuchumi kupitia mikopo nafuu.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Frola Hindi amewataka wanawake kujikomboa kimaisha ili kuweza kutimiza majukumu ya familia amewataka kubadilika na kuzingatia masuala ya kimaendeleo lakini pia amewataka wanawake kuwa na ujasili na kwamba pale wanapofanyiwa ukatili basi kuchukua hatua kufika katika vyombo husika vinavyojihusisha na kusimamia haki za mwanamke.
Akihitimisha sherehe hizo Mh Mariamu Palingo Diwani wa viti maalumu Tarafa ya Saranda amesema kuwa anawashukuru watu wote kwa ushrikiano wao katika maadhimisho hayo lakini pia amewaagiza wanawake kutekeleza yale yote yaliyoagizwa na kuhakiksha wanasimamia kwa ukamilifu ili kupata kizazi chema na chenye uadilifu.
Aidha atika sherehe hizo baadhi ya wadau washiriki kama vile NMB,CRDB,MAHAKAMA,USTAWI WA JAMII,CAMFED na Wadau wengine waliweza kutoa taarifa zao ,na shirika la Cama Member Association kwa kushirikiana na CAMFED waliweza kutoa zawadi za madaftari na kalamu kwa wanafunzi wa shule za saranda zawadi zenye thaman ya tsh 70,000/=.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.