- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, leo tare 14 Agosti 2019 amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Deogratius Ndejembi, Kamati ya fedha na Mipango, kamati ya Siasa na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, lengo likiwa ni kutembelea mradi wa Kilimo cha Pamoja cha Korosho cha Mkwese-Masigati na kujifunza mambo mbalimbali yaliopelekea kufanikisha mradi huu mpaka kwa hatua uliofikia.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa wakati alipowasili katika Ofisi ya Wilayani hiyo katika ziara ya kikazi ya siku moja Manyoni Mkoani Singida. Kushoto ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto)
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg. Charles Edward Fussi wakati alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa na kushoto ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye kofia) akiangalia Shamba lililopo katika kijiji cha Masigati Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiangalia mkorosho uliopandwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Rehema Nchimbi tarehe 18 Januari, 2018 wakati alipotembela Shamba la korosho lilipo katika kijiji cha Masigati Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tukio lililofanyika leo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.