• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara Kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Manyoni District Council
Manyoni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • History
        • Orodha Viongozi
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
      • Mchoro wa Kiutawala
      • Picha Ya Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala & Utumishi
        • Majukumu ya Idara
        • Legal Seatings on Council's level
        • Department Information
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala wa Mazingira na Usafi
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
      • Huduma Zetu
        • Afya
        • Elimu
        • Maji
        • Kilimo
        • Mifugo
        • Uvuvi
    • Kilimo cha Korosho
    • Msimu wa mashamba ya Korosho 2019/2020
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha Ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba Ya Picha
    • Matokeo ya Kidato cha Pili 2018

Taarifa ya kilele cha siku ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani tarehe 1/12/2018 Wilaya ya Manyoni.

Imewekwa Mtandaoni mnamo: December 1st, 2018

1. UTANGULIZI

Siku ya UKIMWI huadhimishwa kimataifa na kitaifa kila mwaka tarehe mosi Disemba, Pendekezo la kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani lilitolewa mnamo mwaka 1988, ikiwa na lengo la kutafakari hali halisi na mwelekeo wa udhibiti wa UKIMWI kimataifa na kitaifa pamoja na kuwakumbuka wapendwa waliofariki na  virusi vya ukimwi. Lengo la kufanya maadhimisho haya katika kata ya Muhalala ni kutokana na muingiliano wa wananchi kutokana na shughuli za kimaendelea zinazoendelea hapa Muhalala.


2. HALI YA MAAMBUKIZI NA UPIMAJI VVU:

Kuanzia Desemba 2017 hadi october 2018 jumla ya watu 25,878 walipima afya zao, Me 12,670 Ke 13,208. Kati ya watu waliopima watu 1,167 walipatikana na maambukizi ambapo Me 474 na Ke 693 sawa na asilimia 4.5%. 

Hali ya maambukizi imeongezeka kutoka 4.4% ya mwaka 2017 novemba na kufikia 4.5% novemba 2018.

Hii inamaaanisha juhudi zaidi za mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU zinahitajika ili kufikia 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wafahamu kuwa wanaishi na VVU, asilimia 90 ya wanaoishi na VVU watumie ARV kwa usahihi na uendelevu na asilimia 90 ya wanaotumia ARV waweze kufubaza  Virusi vya UKIMWI.

Aidha kumekua na vichochezi mbalimbali/ visababishi vinavyopelekea kuongezeka kwa maambukizi mapya ya VVU katika Halmashauri ya Manyoni.

  • Kuimarika kwa miundombinu ya usafiri kunakoleta mwingiliano wawatu
  • Kuhama kwa watu kutoka mikoa mingine na kuja Manyoni kutokana na fursa za kiuchumi kuongezeka hasa kwa vijana balehe na wanawake vijana.
  • Kuwepo kwa migodi na shughuli za UVUVI
  • Ufuasi mbaya wa dawa za ARV (ARV zikitumika vizuri zinasaidia kupunguza maambukizi ya VVU.


3. FAIDA ZA KUPIMA KWA HIARI;

  • Kujua afya yako na kuweza kupanga mipango yako
  • Kunusuru afya ya mama na mtoto  endapo ameathirika
  • Kutoendelea kuambukiza na kupokea maambukizi mapya.

 

4. MATUMIZI YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI   (ARV/ART):

Hadi Novemba 2018 jumla ya wagonjwa 3,355 wanatumia dawa za kupunguza makali ya   VVU ambapo Me 850 na Ke 2505.


5. MAFANIKIO:

  • Kuzindua kampeni ya furaha yangu ambapo kampeni iliwezesha jumla ya watu 750 kupima Me 364 Ke 386 kati ya hao waliokutwa na maambukizi jumla ni 16 Me 7 na Ke 9 ambayo ni sawa na asilimia 2.1%
  • Upimaji wa  virusi vya ukimwi kwa hiari umeongezeka katika jamii
  • Jamii imebadilika kuhusu kukubali hali halisi juu ya matokeo yanayotolewa baada ya kupima.
  • Asasi za kiraia kwa kushirikiana na serikali zimekuwa zikifanya shughuli mbalimbali  kama vile upimaji, utoaji wa rufaa na uundwaji wa vikundi vya watu wenye  VVU katika  shughuli za ujasiriamali


 6. CHANGAMOTO:

  • Umaskini wa kipato unaowafanya vijana/wanawake na wanaume wengi kuingia              katika biashara ya ngono na madawa ya kulevya.
  • Baadhi ya wateja wanaotumia dawa huacha kutumia dawa hivyo kufanya maambukizi kuwa juu yaani ufuasi mbaya wa ARV.
  • Upungufu wa watumishi wenye ujuzi wa kutoa huduma ya tiba na matunzo

     e. Baadhi ya mila na desturi zinazopelekea maambukizi ya VVU kama vile;

  • Ndoa za utotoni
  • Kurithi wajane/wagane
  • Kusafisha/kutakasa wajane
  • Unyago na jando
  • Wanaume kutoshiriki masuala ya haki ya uzazi


         7. MIKAKATI:

  • Kuwaelimisha wateja wanaotumia dawa kutorudia kupima maambukizi ya VVU badala yake wapime CD4  na viral load (Wingi wa virusi)
  • Kuendelea kuomba wahisani waendelee kutoa mafunzo ya utoaji wa ARV kwa watoa huduma
  • Elimu inaendelea kutolewa katika jamii juu umuhimu wa kupima afya.
  • Kutokomeza vitendo vyote vinavyopelekea unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwachukulia wahusika hatua za kisheria.
  • Kuendelea kushirikisha jamii kupitia kamati za Ukimwi za vijiji, Vitongoji na kata katika suala la utoaji wa elimu ya Ukimwi kwa Jamii.
  • Kuendelea kuhimiza wanaume kujitokeza kupima VVU.
  • Kuongeza vituo vitakavyokua vinatoa huduma ya ushauri na upimaji hasa vijijini.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWAAJILI YA SHUGHULI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA September 15, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA MASHAMBA YA KOROSHO MWAKA 2022/2023 July 04, 2022
  • FOMU YA MAOMBI YA MASHAMBA YA KOROSHO MWAKA 2022/2023 July 04, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 12, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBUNI MJIPATIE VIWANJA KWA BEI NAFUU

    May 05, 2025
  • "KIKAO CHA PHC CHAFANYIKA"

    April 26, 2025
  • "Jimbo la Manyoni Mashariki kubadilishwa Jina"

    April 26, 2025
  • "UJUZI UTABADILISHA MAISHA YA WATANZANIA"

    March 23, 2025
  • Angalia zote

Video

Ngoma za asili Siku ya UKIMWI Duniani
video zingine

Kurasa za Karibu

  • About Manyoni
  • Completed Projects
  • Ongoing Projects
  • Primary Schools Students Registration (Prem)
  • Instagram

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • President's Office, Public Service Management
  • Singida Region
  • Necta
  • MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
  • Kupata Salary Slip

Fuatiliaji ya watembezi wa Kidunia

world map hits counter

Kihesabia Watembezi

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI

    Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI

    Simu: +255 26 2540136

    Namba ya Simu: +255 26 2540136

    Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera za Siri
    • Malalamiko
    • Maswali ya Mara Kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.