- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MPANGO wa Tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), awamu ya pili unaoendelea kusaidia kaya maskini umekuwa mkombozi kwa watu wengi hususani wakinamama waliopo Vijijini na kurudisha matumaini yao ya kuendelea kuishi duniani bila ya kuwa na woga wa Maisha yao ya kila siku na pia imeondoa baadhi ya changamoto mbalimbali za kimaisha walizokuwa wakizipitia .
Mpango huo wa Tasaf kwa kaya maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Vijijini ulianza mwaka 2014 kwa utambuzi wa kaya hizo ambazo nyingi zilikuwa zinakabiliwa na matatizo ya mbalimbali ikiwemo kula mlo mmoja kwa siku usiokuwa na uhakika, watoto kukosa elimu, na kukosa makazi ya kudumu huku pia wakikosa vyoo bora hali iliyowafanya kuwa na maradhi mbalimbali iliwafanya waishi maisha ya wasiwasi yasiyokuwa na matumaini.
Baada ya kaya hizo kuingia katika mpango wa ruzuku za Tasaf kwa wanufaika, asilimia kubwa ya kaya hizo wamejikwamua kiuchumi na kuweza kupata mahitaji yote muhimu ambayo walikuwa wakiyahijati kwa muda mrefu bila mafanikio.
Hata hivyo, licha ya wanufaika hao kwa kiasi fulani kufanikiwa kujikwamua kiuchumi ambapo sasa wanaweza kupata chakula cha uhakika kwa milo mitatu kwa siku, makazi ya kudumu, kujiingiza katika ufugaji ikiwa ni pamoja kuanzisha biashara mbalimbali bado kuna wanufaika wengine hawajaweza kutumia fedha hivo kuzalisha hali inayosababisha wakate tamaa na malengo yao na kuonyesha kuwa bado hawezi kuishi bila ya ruzuku za TASAF.
Wasiwasi huo unatokana na wanufaika hao kutokuwa na elimu ya ujasiliamali ambayo ingeweza kuwapa elimu ya kufanya biashara zao kitaalam na kuweza kusimamia fedha zinazotokana na biashara, kilimo na ufugaji na kuwawezesha kuwakwamua zaidi ya walipo sasa.
Akizungumza hivi karibuni na Afisa Habari aliyetembelea katika kata hiyo ili kuweza kujionea jinsi ambavyo wanufaika hawa wameweza kunufaika na mpango huo. Tatu Rashidi mama mwenye Watoto 4 kutoka katika Kijiji cha chikola na kata Chikola iliyopo katika Halmashauri hii ya Chikola anaonyesha furaha na tabasamu ambalo linaviashiria vya matumaini ya Maisha kutokana na kupata fedha kutoka mpango huu wa Tasaf mfuko wa uwezashaji wa watu wenye uwezo mdogo yaani kaya maskini.
Tatu anasema kuwa alijiunga na mpango huu wa Tasaf mwaka 2014 Na kwamba alikuwa akipokea tsh 48000, ikaja ikapungua akawa akipata tsh 26000, na hadi kufikia sasa anapokea tsh 46000 amabazo zinamsaidia anasema kuwa wakati anajiunga Maisha yake yalikuwa ya shida sana yeye pamoja na Watoto wake alikuwa akipata mlo mmoja kwa siku wakati mwingine alikuwa hawezi kabisa kumudu Maisha anasimulia kuwa hakuwahi kuwaza kabisa hasilani kuwa na yeye siku moja angeweza kuwa jinsi alivyo anasema kuwa Tasaf imemnufaisha sana.
Ninayo furaha kubwa kwani kwa sasa ninafuga kuku ninafuga mbuzi Watoto wanasoma na wengine wamefika mpaka Sekondari na Tasaf imenisaidia mpaka sasa nimechaguliwa kuwa katibu Mwenezi wa chama kutokana na muonekano wangu kwa kweli tunashukuru sana mpango huu umeokoa kaya nyingi sana hapa kijijini kwetu anasema kwa furaha kubwa Tatu Rashidi
Baada ya fedha hizo kuongezeka ikawa sasa napeleka kidogo shambani halafu nikawa natoa kidogo napeleka kwenye ujenzi maana nilikuwa naishi kwenye nyumba ya tope ambayo Ilikuwa karibu inaniangukia.nilifanikiwa kujenga nyumba ndogo na kutoka kwenye nyumba hiyo baada ya kuzalisha faida na kuwalipia watoto ada za shule.nawashukuru sana Tasaf.
Aidha amewaasa walengwa wenzake ambao nao wanapata Ruzuku ya Tasaf kuzitumia fedha hizo katika kujikwamua kiuchumi na siyo kwenda kulewa pombe kwani pombe inapunguza afya yao, inamaliza hela bila kujua ulipomalizia zinakufanya mpaka unasahau, yaani kuna mtu anaenda kunywa pombe na akishaenda kunywa atahakikisha anakunywa mpaka aimalize ile hela mkononi. Tatu ameongeza kuwa kuna wengine wakipata fedha hizo wananunua wax ili waonekane na watu badala yake waizalishe au kutafuta namna ya kuibua miradi ambayo itaweza kuwasaidia.
Naye Maria ni miongoni kwa wanufaika ambao wamefanikiwa kujikwamua katika maisha ya awali kutoka kutopata mlo hadi kuwa na uhakika wa chakula na kuweza kujenga nyumba ya kudumu ya kuishi ambayo anaeleza kuwa alipojiunga na mpango huu wa Tasaf aliweza kuzalisha kiasi hicho anachopata kwa kununua mbogamboga na kuuza kisha kijiwekeza faida na hatimaye alianza kufyatua tofali na kujenga nyumba yenye vymba vitatu na sebule ambayo kwa sasa imefikia hatua ya renta.
“Hii hela tunayopata inasaidia endapo mtu atakua na njia ya kuizalisha kama ambavyo sisi tunafanya kuna njia nyingi za kuizalisha kama vile kufuga kuku kuuza mayai au kuzalisha wale kuku au biashara nyingine ndogondogo kama vile kupika maandazi hakika mtu unazalisha kwani Haba na haba hujaza kibaba hivyo nami niwashauri walengwa kuizalisha tu”.alifafanua Maria
Naye Mratibu wa Tasaf Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Christopher Nkui amewataka walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Tasaf kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu katika kufanya kazi na kutafuta namna ya kuizalisha ili waweze kupunguza hali ya umaskini katika maeneo yao .
Nkuhi ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuweka mazingira mazuri kwa wananchi ili waweze kujiletea maendeleo na kuboresha Maisha yao .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedeck Humbe amewataka walengwa kutobweteka na mafanikio waliyoanza kupata kutokana na huduma zinazotolewa na Serikali kupitia Tasaf badala yake waendelee kuupiga vita umaskini kwa vitendo kwa kuongeza juhudi katika kazi za uzalishaji ili hatimaye awaweze kuboresha Maisha yao kwa kiindi hicho
Aidha Humbe ameongeza kuwa walengwa wanapaswa kutambua kuwa ruzuku hizi zina muda na baada ya hapo mlengwa anakuwa na ukomo hivyo basi wahakikishe wanazitumia vizuri ili ziweze kuwaletea manufaa na si majuto.
Humbe amewaagiza kuacha kuzitumia fedha hizo kwa mambo ambayo si ya kimaendeleo kama vile kuoa mke wa pili kwa upande wa kina baba wanaopata fedha hizi na kwa wakina mama kuacha kuwaza kuvaa waxi na mengineyo yasiyokuwa na faida bali watumie fedha hizo kuboresha Maisha yao kama vile kupeleka watoto shule kuibua miradi itakayo weza kuwasaidia pindi watakapofikia ukomo wa kupokea ruzuku hiyo.
Katika hatua nyingine Humbe amewaagiza Maafisa maendeleo na wawezeshaji wa mpango huu kuwa na utaratibu wa kuweza kuwafuatilia walengwa hao na kuendelea kuwapa elimu ya kujitegemea na kuibua miradi ambayo itaweza kuwanufaisha walengwa hao
Ameongeza kuwa Tasaf inagusa Nyanja muhimu za maendeleo ya wananchi katika sekta mbalimbali za maji ,uchumi,kilimo,mifugo na nyingine nyingi ambazo kwa ujumla wake zinagusa Maisha ya wananchi wengi moja kwa moja
“kumekuwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji shughuli hii yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na kwakiwango kikubwa imesaidia kuboresha Maisha ya wengi” alisema HumbeMSIBWETEKE.pdf
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.