- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 14 Aprili 2023 Timu ya Wataalamu imefika wilayani Manyoni kufanya Tathimini ya Athari ya Mazingira kabla ya ujenzi wa chuo cha VETA kuanza,Wataalamu hawa wameanza na kikao cha ndani na Wakuu wa Taasisi mbalimbali na wakuu wa Idara na vitengo ambao ni wahusika kwenye kufanya tathimini hii kisha kutembelea Eneo ambalo Chuo hiko kinakwenda kuanza Ujenzi wake.
Dkt. Richard Kimwaga Mhadhiri Mkuu Chuo Kikuu cha Dar-es-salam ameongoza timu hiyo ya Wataalamu kufanya thatmini ya athari hizo za kimazingira kabla ya kuanza rasmi ujenzi wa Chuo cha VETA. Kwenye Timu hii ya kufanya Tathimini ya Athari za Mazingira wamefika wahandisi wawili wa Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Mhandisi Nuhu Moto na Mhandisi Evody T. Ndumiwe.
Dkt Kimwaga amesema ”Ni matumaini yangu kuwa wote tunafahamu kuwa Wilaya ya manyoni ni Miongoni mwa Wilaya zilizopata fedha kwaajili ya Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha VETA hivyo najua mmeupokea na mtakua tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mradi huu wa ujenzi wa VETA unakamilika kwa wakati na ukiwa na Ubora na viwango vinavyotakiwa”.
Tuendelee kutambulisha na kuhabarisha Umma juu ya uwepo wa Mradi huu lakini pia kuomba ushirikiano kwa jamii lakini pia kuwaeleza umuhimu wa uwepo wa Chuo hiki katika Mazingira yetu na zaidi ya yote kuwaomba kushiriki shughuli za ujenzi wa Chuo hiki.Alisisitiza Dkt Kimwaga.
Naye Ndg Elias Moleli Afisa Maendeleo Halmashauri ya Manyoni kwa Niaba ya Mkurugenzi amesema; “Tunaufahamu Mradi huu na tumeupokea na Kwa niaba ya Halmashauri ya Manyoni ninawahakikishia tutashiiki kikanilifu ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati ukiwa na ubora wa hali ya juu”
“Tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Raisi wake Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuhakikisha Wilaya zote zinapata chuo cha VETA lakini zaidi ya yote kuridhia Wilaya ya manyoni kuwa miongoni mwa Wilaya iliyopata mradi huu wa ujenzi wa VETA kwa awamu ya kwanza hakika Tunashukuru sana.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.