- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Joseph Serukamba ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) kuhakikisha wanamaliza tatizo la Wanyama wakiwemo Tembo kuvamia Makazi na Mashamba ya Wananchi Wilayani Manyoni.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Serukamba amesema hayo katika Vijiji vya Mpapa, Simbanguru na Nkonko wakati akisikiliza Kero za Wananchi hao .
Wananchi wa maeneo hayo wamesema kuwa kwa kipindi kirefu Wanyama hao wamekuwa wakivamia Makazi na kula nafaka ikiwemo mahindi aidha kwa kipindi cha Kilimo, Tembo uharibu Mashamba na wakati mwingine kusababisha majeruhi na vifo kwa Wananchi.
Kwa upande wake Herman Nicholaus Nyanda - Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi - Kanda ya Kati -TAWA amesema Serikali kupitia TAWA wameendelea Kufanya jitihada za kuwafukuza Tembo pindi wanapopata Taarifa za uvamizi wa Wanyama katika Makazi na Mashamba ya Wananchi.
Aidha Serikali imekuwa ikitoa kifuta machozi na kifuta jasho kwa wananchi wanaharibiwa mazao, majeruhi na Vifo vinavyotokana na Wanyamapori hao.
Kamishina Nyanda amesema Jeshi la Uhifadhi Kanda ya Kati wametoa na inaendelea kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya kujilinda na kuzuia Tembo kutofika katika maeneo ya Mashamba na Makazi ikiwemo kulima na kutumia pilipili, oili chafu na kuchimba mifereji ili kupunguza athari za Wanyamapori hao. Sambamba na hilo TAWA imeendaa Mafunzo Maalumu kwa Vijana waliopitia Jeshi la Akiba Kwa Kila kijiji ili wapewe Mafunzo Maalumu ya kulabiliana na Wanyamapori wakali na waharibifu ikiwemo Tembo.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Joseph Serukamba ameendelea na ziara ya kijiji kwa Kijiji ambapo katika maeneo hayo amekuwa akipokea na kutatua Kero za Wananchi, Kufikisha Salamu za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na kukagua miradi ya Maendeleo Katika Vijiji vyote vya Mkoa wa Singida.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.