- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Suleiman Mwenda tarehe 21 oktoba 2022 amefungua warsha ya siku tatu ya mafunzo,majadiliano na kuweka mkakati juu ya namna nzuri ya kuimarisha uhifadhi kwenye mapori ya Rungwa, Muhesi na Kizigo inayofanyika katika ukumbi wa Cassanova uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Warsha hii imehudhuriwa na Wadau kutoka maeneo mbalimbali yani Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya , Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida ikijumuisha Halmashauri zake mbili (Manyoni na Itigi) na Wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora.
Wageni kutoka TAWA walipowasili Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Manyoni wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi (TAWA) Ndg Mabula Misungwi Nyanda anayesaini kitabu cha Wageni.
Nakupongeza Kaimu kamishna na kamati yako kwa kuitisha warsha hii ya wadau mbalimbali yenye nia ya kuimarisha uhifadhi katika mapori ya Rungwa, Kizigo na Muhesi yaliyopo katika maeneo yetu.Na kama tunavyojua hifadhi ni moja ya kivutio kikubwa katika nchi yetu na kinanyanyua uchumi wa nchi yetu,
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Suleiman Mwenda akiwasili katika viwanja vya Ukumbi wa Cassanova.
Naye Kaimu Kamishna wa Uhifadhi (TAWA) Ndg Mabula Misungwi Nyanda Alisema, Jukumu la Kulinda Wanyama katika Mapori yanayotuzunguka ni la Kwetu sote wadau, Na pindi Wanyama wakali na waharibifu wanaofika maeneo ya makazi lazima tuwaelekeze namna nzuri ya kupunguza changamoto hii na ndio maana tumeandaa warsha hii ili mpate mafunzo mbalimbali na tupate changamoto zinazowakabili nyie ambao mnaishi karibu na hifadhi na mwisho kwa pamoja tuweke mikakati ya kuimarisha uhifadhi na kutatua changamoto hizo.
Wadau mbalimbali waliohudhuria warsha ya Uhifadhi
Mkufunzi akiendelea kutoa elimu kwa wadau wa uhifadhi waliohudhuria warsha.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.