- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
TRA Manyoni Yaendesha Semina kwa Wafanyabiashara Kuhamasisha Ulipaji Kodi kwa Hiari
*Manyoni, 20 Agosti 2025 – Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, imeendesha semina maalum kwa wafanyabiashara na wadau wa masuala ya kodi, kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu wajibu wao katika ulipaji wa kodi na mabadiliko ya sheria mpya za kodi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
wafanyabiashara wote kushirikiana kwa karibu na Mamlaka hiyo kwa kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari, akisisitiza kuwa ulipaji kodi kwa hiari ni njia bora ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
“TRA inaendelea kuimarisha uhusiano na walipakodi kwa njia ya majadiliano ya wazi, elimu na msaada wa karibu. Tunahamasisha ulipaji kodi kwa hiari kama msingi wa maendeleo ya Taifa,” alisema Bw. Pancras.
Katika semina hiyo, Maafisa wa TRA Bw. Jamal Ngarawa Afisa msimamizi wa kodi kutoka TRA makao makuu na Bw. Zephania Mange walitoa elimu ya kina kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi yaliyoanza kutumika katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, ikiwemo taratibu mpya za usajili, ulipaji na marejesho ya kodi kwa njia za kidigitali.
Washiriki wa semina hiyo walipata nafasi ya kuuliza maswali, kutoa maoni na kupokea ufafanuzi wa moja kwa moja kutoka kwa maafisa wa TRA, jambo lililosaidia kuongeza uelewa na kuondoa sintofahamu kuhusu baadhi ya masuala ya kikodi.
Semina hiyo ni sehemu ya mikakati ya TRA kuendelea kuelimisha, kushirikiana na kujenga uaminifu na walipakodi, kwa lengo la kuongeza mapato ya serikali kwa njia shirikishi na yenye tija.
@tratanzania @anastaziatutuba @drmashinjivincent @singidars @tembo_digital_tv @ortamisemi @msemajimkuuwaserikali
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.