- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota kwenye kikao cha Tathimini ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika tarehe 10 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“Niwaombe sana kuchukua Tahadhari juu ya Ugonjwa wa Mlipuko wa Kipindupindu ulioripotiwa katika mkoa wetu wa Singida, Nawaaagiza watumish i wa Afya wa Halmshauri ya Wilaya ya Manyoni kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo wa mlipuko kwa kuzigatia kanuni na taratibu za afya ili kuepukana na ugonjwa huu”.
“Wananchi wepewe elimu juu ya kujenga vyoo bora na matumizi sahihi ya vyoo hivyo, lakini pia kuwa na vifaa maalumu vya kunawa mikono vizuri kwa maji tiririka baada ya kutoka chooni hii itasaidia sana kupunguza uwezekano wa jamii yetu kukumbwa na magonjwa ya mlipuko” Alisisitiza Mhe. Kemirembe.
Mhe. Kemirembe amesema “Wananchi wazingatie usafi wa mazingira kwa ujumla katika maeneo yao wanaoishi na kuepuka kufanya shughuli zao za kijamii karibu na vyanzo vya maji kwani hili ndio tatizo kubwa litakalofanya jamii kupata magonjwa ya mlipuko kwani kufanya shughuli mbalimbali karibu na vyanzo vya maji huchafua vyanzo vya maji na kupelekea jamii kutumia maji yasiyo safi na salama”
Sambamba na Hilo Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota Ameendelea kusisitiza suala la Lishe bora kwa jamii na kuhakikisha wanafunzi waliopo shule wanapata chakula mashuleni kwa kuwataka Watendaji wa kata kuhakikisha shule zote za sekondari na za msingi wanakuwa na eneo lao maalumu kwaajili ya kilimo ili kujipatia chakula chao.
“Pamoja na wazazi kuchangia chakula mashuleni watendaji wa kata hakikisheni shule zote za sekondari na za msingi wanakua na eneo lao walime vyakula ambavyo watavitumia wao wenyewe wawapo shuleni hii itasaidia sana na itapungza uhitaji mkubwa wa vyakula kutoka kwa wazazi”
“Mwisho niwaombe sana Twendeni tukatimize wajibu wetu kwa kuhakikisha tunawahudumi wananchi wetu vizuri, kwa kauli nzuri zitakazofanya waamini Serikali yao ya Awamu ya Sita chini ya Mama yeu Dkt Samia Suluhu Hassan inawapenda na kuwajali, Sitamvumilia Mtumishi atakaetoa huduma kwa wananchi kwa kauli na lugha chafu” Alisisitiza Mhe. Kemirembe.
Naye Ndg. Fadhili Chimsala kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni alisema “Niwashukuru wote mliohudhuri kikao hiki naamini kwa pamoja yote tuliyojadili tunakwenda kushirikina ili kufanikisha yote, Mimi na Timu yangu ya wataalamu wa Idara ya Afya na Watendaji wengine tunakwenda tunakwenda kuhakikisha tunatoa elimu kwa wananchi wetu vizuri juu ya masuala haya ya Afya ili jamii yetu ibaki kuwa salama wakati wote.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasilino Serikalini
Halmashauri ya Wikaya ya Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.