- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Magdalena Dinawi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya tarehe 04 Juni 2024 walipofika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni akiwa ameambatana na Timu kutoka Wizara ya Afya, Tamisemi na Ofisi ya Rais Ikulu kutoa Elimu juu ya kupambana na Magonjwa ya Mlipuko (Kipindupindu)
Kipindupindu ni ugonjwa hatari unaosababishwa na viini vinavyoenezwa kupitia kwa kinyesi. Kipindupindu husababisha kifo kati ya masaa matatu au manne mgonjwa akikosa kutibiwa kwa haraka.
Mtu anaweza kupata kipindupindu kutokana na kunywa maji au kula vyakula vilivyochafuliwa na viini hivi.
Dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni chache na ni rahisi kwa mtu kuweza kuzibaini na zinaweza kuonekana ndani ya masaa machache au siku tano baada ya maumbukizi. Dalili hizo ni:
1:Kuharisha maji maji yanayofanana na maji ya mchele
2:Kutapika
3:Kujisikia mlegevu, kukosa nguvu
4:Wakati mwingine kusikia maumivu ya misuli
5:Upungufu wa maji mwilini
6:Kuna wakati mgonjwa anakuwa na ngozi iliosinyaa na mdomo kukauka
"Tuendelee kuchukua tahadhari kupambana na Magonjwa ya Mlipuko kwa kuhakikisha tunafata taratibu zote za Afya yani kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono kwa maji tiririka, kujenga vyoo bora na kuvitumia vizuri na kuhakikisha mazingira yanayotuzunguka yanakuwa safi"' Alisisitiza Bi Magdalena
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.