- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa leo tarehe 06 januari 2023 na Afisa Elimu Msingi Ndg Hamisi Milowe kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyonii katika kikao cha maandalizi ya uzinduzi wa upandaji miti kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kilichohudhuriwa na Wadau mablimbali wa Mazingira.
“Tutunze mazingira kwa kuhakikisha tunapanda miti katika maeneo yetu, maeneo yetu mengi yapo wazi hivyo ni athari kubwa kwa Maisha yetu kwani tunaweza kukos hali ya hewa nzuri na pia kukosa mvua kabisa hivyo tuelimishe jamii juu ya umuhimu wa upandaji miti ili wawee kupanda miti kwenye maeneo yao
Wananchi wamekata miti sana ili kupata makazi na hata maeneo kwaajili ya shughuli za Kilimo hivyo maeneo yamebaki wazi bila miti, sasa tunakwenda kuanza kampeni rasmi ya kupanda miti kwenye maeneo yetu ili sasa kuboresha mazingira yetu na kuepuka madhara yatokanayo na mazingira kukosa miti”.
Ninawategemea sana katika zoezi hili la upandaji miti, Wenyeviti wote hakikisheni maeneo yenu yote yaliyowazi yanapandwa miti ili kufanikisha zoezi hili, tusimamie hili na tuwaelimishe wananchi wetu kuwa na hulka ya kupanda miti katika maeneo yao ya makazi ili kuboresha mazingira.
Naye Afisa Misitu Halmashauri Ndg Freedon Kikasi amesema; Kuanzia kesho tarehe 07 januari mkoa wa Singida katika kila wilaya tutakua na Uzinduzi wa upandaji miti hay ani Maagizo ya mkuu wetu wa Mkoa na katika mkoa mzima tunatakiwa kupanda miti Milioni 5, Hivyo niwaombe sana viongozi ushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa asilimia zote.
Tupande miti ili kurekebisha mandhari lakini pia ili kuepusha madhara yatokanayo na ukosekanaji wa miti,madhara ya kukosekana kwa miti hayatokei pale pale madhara yanatoke taratibu hivyo tujitahidi kuzuia madhara hayo. Amesisitiza Ndg Kikasi.
Ndg Kikasi amesema;Kila kaya Ipande Miti minne(4) kila mwaka na viongozi hakikisheni kwenye barabara zetu na kuzunguka vyanzo vya maji miti inapandwa lakini pia kwenye ofisi zote za Serikali kunakua na miti ya kutosha na itunzwe ili ikue. Wenyeviti wa vitongoji sisitizeni hili na waelimisheni wananchi juu ya hili.
Maeneo ambayo yatakua hayana miti na vyanzo vya maji ambavyo vitaharibika kwa kukosa miti nitaanza na viongozi wa maeneo husika kwasababu leo tumeitana kuelekezana ili mkayafanyie kazi na kuhakikisha tunafanikiwa kubadili mandhari ya maeneo yetu. Vyanzo vya maji vipandwe miti na mabango yawekwe kuonesha hiki ni chanzo cha maji ili sasa watakaoharibu wawajibishwe. Amesisittiza Ndg Kikasi
Halmashari zinatunga sheria za kulinda na kutunza miti yote inayopandwa ( Sheria ndogo za kusimamia Mazingira) Lakini pia zitaweka sheria kwa wale ambao hawataki kusiriki zoezi la kuapanda miti katika maeneo yao, Hivyo niwaombe viongozi na wananchi kwa ujumla kuunga mkono zoezi hili ili tufanikiwe kuboresha mazingira yetu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.