- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 23 machi 2023 Timu kutoka Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni imetembelea Kijiji cha Lusilile kilichopo kata ya Kintinku Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kutambua Eneo ambalo litatumika kujenga Chuo cha VETA ikiwa ni Miongoni mwa Vyuo 63 vitakavyojengwa Nchini Tanzania.
Kaimu Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg.Peter Noel Foya ambaye pia ndiye amepewa madaraka ya kusimamia mradi na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (WYEST) aliwajulisha viongozi wa Kijiji cha lusilile kuwa lengo la Ziara yake ni kutambua eneo la utekelezaji wa mradi wa kujenga chuo cha VETA pamoja na kutambua mipaka.
“Leo nimekuja na Timu yangu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule ili kuona eneo mlilolitenga kwaajili ya kujenga Chuo cha VETA na kutambua zUkubwa wake pamoja na Mipaka ya eneo hili”
Ndg Foya alisema, Mradi huu wa Ujenzi wa Chuo cha VETA utakuwa awamu mbili (2)ambapo awamu ya kwanza zimetolewa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.4 ili kuanza kujenga Miundombinu ya majengo 9 ambayo ni : Jengo moja la utawala, jengo moja la darasa, kibanda kimoja cha mlinzi, nyumba moja ya Mkuu wa Chuo,jengo la karakana tatu(3), jengo moja la choo na jengo moja la umeme.
Kwa ngazi ya taifa vitakuwa vyuo 64 ambapo vyuo 63 vitakuwa katika ngazi ya wilaya na chuo kimoja(1) ngazi ya mkoa ambapo kitajengwa katika mkoa wa SONGWE na kwa SINGIDA wilaya zilipatiwa mradi ni Manyoni, Iramba na Mkalama hivyo kipekee Tunamshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutupatia mradi huu katika Wilaya ya Manyoni.Alisisitiza Ndg Foya.
Ndg Foya amesema, Mradi utatekelezwa kwa kutumia FORCE AKAUNTI na kuanzia tarehe 27/3/2023 matangazo ya zabuni yatakuwa yametoka pamoja na taratibu za manunuzi na Ujenzi utaanza mwezi APRIL hadi SEPTEMBER 2023.
Mshauri mwelekezi wa mradi ambaye ameteuliwa na wizara ya elimu kwa utekelezaji wa mradi wa wilaya ya Manyoni atatoka BICO( Bureau of Industrial Cooperation) kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo niwaombe kutoa ushirikiano wa Kutosha pindi tutakapoanza Mradi wa Ujenzi wa Chuo hiki cha VETA katika Wilaya yetu ya Manyoni.alisisitiza Ndg Foya.
Naye Afisa tarafa ya Kintinku Ndg. Charles Andrew Magesa amesema,Ninaishukuru sana Serikali ya Awamu ya sita chini ya Raisi wake Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutupati amradi huu katika Wilaya ya Manyoni na cha zaidi nashukuru kwakua mradi huu unakwenda kutekelezwa ndani ya tarafa yangu ya Kintinku ,Tunashukuru kwa kupatiwa mradi mkubwa na wenye tija kwa vizazi vijavyo.
Ndg Magesa alisema, Kijiji hiki cha Lusilile kata ya Kintinku kimetenga hekari 48.7 kwaajili ya Mradi huu na niwaombe tulitembelee eneo hili ili kujirizisha na kuona Mipaka.
Sambamba na Kutembelea Eneo hilo na kuliona na kutambua mipaka Ndg Elizabeth Edward Mchele mwakilishi wa Afisa Ardhi wa Wilaya ya Manyoni ameweka alama kwenye eneo hilo la ujenzi na kuwahidi kuwa Maafisa Ardhi Wilaya ya Manyoni watakuja kuchukua vipimo halisi vya eneo siku chache zijazo kabla ya ujenzi wa mradi kuanza.
Katika ziara hiyo ya Utambuzi wa Eneo la Ujenzi wa Mradi viongozi mbalimbali walishiriki HUSSEINI KAlESO- Mwenyekiti wa Kijiji lusilile, HALIMA SEIF- VEO Kijiji cha lusilile, MAGRETH MASAMI- WEO kata ya kintinku,IMANI SAMWEL LECHIPYA-Mhasibu wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule,RAYMOND ERICK MWASHALAWE-Afisa Ugavi Idara ya Uthibiti Ubora,ALBERT CHILUMATE- Mwenyekiti wa Bodi ndogo ya zabuni.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.