- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Uzinduzi wa Mtuli Cup Kata ya Chikola Watikisa Vijana Wahamasishwa Kung’ara kwa Ajira Kupitia Mpira
Chikola, 21 Agosti 2025 Viwanja vya Shule ya Msingi Chikola vililipuka kwa shangwe, nderemo na hamasa kubwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Mtuli Cup, ligi ya soka inayowaleta pamoja vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Kata ya Chikola kwa lengo la kukuza vipaji na kutoa fursa kwa vijana kujitangaza kisoka.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Chikola, Willam Nsajigwa Mwakanyamale, ambaye alifungua mashindano hayo kwa hotuba yenye msukumo mkubwa kwa vijana. Akizungumza mbele ya mamia ya mashabiki na wachezaji, Mwakanyamale alitangaza zawadi kwa washindi watatu wa juu katika ligi hiyo na kuwataka vijana kucheza kwa bidii na nidhamu, kwani ligi hiyo ni sehemu ya tathmini ya kuchagua wachezaji wa kushiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Manyoni.
Nia si tu ushindi, bali ni nafasi ya kujitangaza kisoka, alisema.
Kwa upande wake, James Mtuli, mthamini mkuu wa kombe hilo, alieleza dhamira yake ya kusaidia kukuza vipaji vya vijana kupitia mashindano hayo. “Mpira si burudani tu, ni ajira halali na njia ya kubadilisha maisha. Nimeamua kudhamini Mtuli Cup ili kuona vipaji vinang'aa kutoka Chikola hadi taifa zima,” alisema Mtuli kwa msisitizo.
Mashabiki walifurika kwa wingi kushuhudia mechi ya uzinduzi ambayo ilionesha ushindani mkali, hamasa na vipaji vya hali ya juu kutoka kwa vijana wa Chikola. Mtuli Cup imeonekana kuwa si tu mashindano ya mpira, bali jukwaa la matumaini kwa vijana waliokuwa wakisubiri fursa ya kuonekana.
Ligi hiyo itaendelea kwa wiki kadhaa, ikihusisha timu mbalimbali ndani ya kata, huku matarajio makubwa yakiwa ni kuibua nyota wapya wa soka kutoka Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.