- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndugu Charles Edward Fussi amezindua Semina ya mafunzo ya usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa mtoto walio chini ya miaka mitano (Under five birth registration program) Mpango ambao unalenga kuongeza idadi kwa kiasi kikubwa cha Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano, sambamba na kuboresha mfumo wa usajili Tanzania Bara.
Ndg Charles Fussi amesema kuwa Shughuli hii hapo awali ilikuwa ikifanyika katika ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya na sasa usajili huu umehama kutoka serikali kuu kwenda ofisi za serikali za mitaa. Utekelezaji wa mfumo huu utafanyika kwa mifumo ya afya na serikali za mitaa iliyopo
Usajili huu ni muhimu kwasababu utamsaidia mtoto kupata cheti cha kuzaliwa bure kabisa na Cheti cha kuzaliwa kitamsaidia mtoto katika mambo mbaliambali ikiwemo kumpa mtoto utambulisho wa awali, Kitamuwezesha Mtoto kupata elimu na maisha bora ambapo pamoja na kwamba ni haki yake na kitaweza kumlinda katika kuzuia ajira lakini pia kitampa uwezo wa kuendelea kupata utambulisho zaiddi katika kutambua utaifa wake kwenye kitambulisho cha taifa n ahata kupata hati ya kusafiria.
Katika zoezi hili la kusajili na kutoa vyeti Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ina lengo la kuwafikia watoto Zaidi ya 38000, zoezi ambalo limepangwa kufikiwa ndani ya siku 12 za kampeni ambayo itaanza rasmi tarehe 15 March 2019 na litafanyika katika vituo 52, zikiwemo ofisi za kata 19 na Vituo vya tiba 33 na litafanyika katika vijiji vyote 58 vya halmashauri ya Wilaya ya Manyoni panoja na mamlaka ya mji mdogo wa Manyoni.
Zoezi hili linategemea kusajili Watoto kwa asilimia kubwa ukilinganisha na usajili wa kawaida wa uliokuwepohapo awali ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana usajili ulifanyika na kutoa vyeti kwa Watoto kwa 13%
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.