- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Manyoni iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni waaswa kutojihusisha na vitendo vya uhalifu kama vile uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya wizi na mengneyo kipindi wakiwa uraiani wakisubiri matokeo yao kwaajili ya kuendelea na masomo.
Haya yamesemwa na Kamanda wa polisi wilayani hapo, Mrakibu wa polisi Ndg Ahmad Makere, leo tarehe 15 oktoba 2022 alipokua mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kuwaaga kidato cha nne Shule ya Sekondari Manyoni.
Mgeni rasmi akizungumza na wazazi,wahitimu , walimu na wengine waliohudhuria mahafali hayo.
Pia Makere amewaasa wazazi kuwa mstari wa mbele kupinga unyanyasaji kwa watoto wote katika jamii inayotuzunguka na kuhakikisha wanawasimamia watoto wao katika maadili mema kwa kipindi chote watakachokua nyumbani kwani jukumu la malezi bora kwa watoto ni la wazazi na walezi.
Ninawapongeza wahitimu wote kwa hatua mlipofikia na ninawasihi kwa muda uliobaki basi ongezeni bidii zaidi kusoma ili mfanye vizuri kwenye mitihani yenu ya mwisho na ninaahidi kutoa jezi za mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana na mpira mmoja kwaajili ya shule kwani michezo hukuza akili kwa watoto. Alisema Makere
Mwisho Mgeni rasmi alipata fursa ya kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo maalumu kwaajili ya wanafunzi wa kike kubadili “taulo za kike” kwa kipindi ambacho watakua shuleni na pia aligawa zawadi maalumu kwa wanafunzi mbalimbali waliofanya vizuri katika Nyanja mbalimbali kama vile masomo,michezo ,usafi,nidhamu n.k
Mgeni rasmi akigawa zawadi mbalimbali kwa wahitimu waliofanya vizuri
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.