- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Manyoni wamesisitizwa kuzingatia urejeshaji wa mikopo yao kulingana na muda waliopangiwa kwenye makubaliano yao ili fedha hizo ziweze kuhudumia wahitaji wengine kwa wakati.
Hayo yamesemwa leo februali 8, 2021 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg. Charles Fussi wakati akifanya kikao na viongozi wa Vikundi vya wajasiriamali ambavyo viliwahi kukopeshwa na vinavyotarajia kukopa, vilivyokamilisha marejesho na ambavyo havijakamilisha marejesho ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa wanufaika wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya halmashauri ya wilaya ya Manyoni.
Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na maafisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mkaguzi wa ndani wa halmashauri na Maafisa wa maendeleo ya Jamii ambao ndio waratibu wa vikundi vya ujasiriamali, Wanavikundi hao wamesisitizwa kuitumia vizuri ofisi ya Maendeleo ya jamii ambayo ndio mlezi wao katika shughuli mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto zao ili kuhakikisha fedha ya serikali inaleta tija kwao na inarejeshwa ndani ya muda husika..
Katika kikao hicho pia wanufaika walipata elimu juu ya masuala mbalimbali ya kuepukana na vitendo vya rushwa, zikiwemo hatua mbalimbali za kufuata katika kupata mikopo hiyo, Elimu ya uendeshaji biashara, Utunzaji wa fedha, matumizi sahihi ya mikopo, vigezo vya utoaji mikopo ambapo pia walijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanufaika hao.
Pamoja na hayo, wanufaika wa mikopo pia walisisitizwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya ilioboreshwa (CHF) ili kuepuka gharama za matibabu za hapo kwa hapo katika hospitali,vituo vya Afya na zahanati
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.