- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Walimu mnatakiwa kuhakikisha mnatekeleza majukumu yenu kwa bidii kubwa na weledi wa hali ya juu kwa kufata miongozo kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuleta matokeo chanya katika taasisi zenu”.
Haya yamesemwa na Bi Leila Sawe Afisa Tawala Wilaya ya Manyoni Muwakilishi wa Mh Mkuu wa Wilaya ya Manyoni leo tarehe 30 septemba kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa kisheria wa Chama cha Walimu (CWT) uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Bi Leila Sawe Aliserma “Wiki ijayo tarehe 5-6 oktoba tunakwenda kuanza mitihani ya darasa la saba hivyo tuisimamie kwa kuzingatia miiko ya mitihani yan kanuni na taratibu na sheria za mitihani kwa kufanya hivyo wote tutakua salama” .
Pia tuwe mabalozi wazuri wa kuyasema yale ambayo Raisi wetu wa awamu ya sita Mh Samia Suluhu Hassan anayafanya kwa kuleta fedha kwaajili ya madarasa na miundo mbinu mingine ili kuhakikisha kuna mazingira rafiki ya utendaji kazi.
Aidha, mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Singida ,Hamisi Mtaturu nae alikua na haya ya kusema ”Tukasimamie mitihani kwa kipindi hichi cha mitihani na sio tuwe sehemu ya wafanya mitihani na Kama chama kwa kuwa mmetuamini na kutuchagua tutahakikisha tunasimamia haki zenu walimu na tunatatua matatizo yenu kwa wakati ili muone faida ya chama chenu. Pia nawaasa msidai Rushwa wakati wa kutimiza majukumu yenu kwani kufanya hivyo ni kukiuka kanuni sheria na taratibu zilizowekwa na Nchi.
Gwamaka Mwakanyamale, Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Manyoni nae alisema “Nawashukuru Wakurugenzi wa Halmashauri zote yani Itigi na Manyoni kwa kutujali na kututhamini na kushirikiana na sisi kwenye mambo mbalimbali kwenye Taasisi zetu lakini pia kwenye mambo ya kijamii kama misiba ya watumishi wenzetu, Tunaomba muendelee na Moyo huo. Pia nawashauri walimu kujiunga na Mwalimu Commercial Bank (MCB) kwani ndio bank yao na kukua kwa banki hiyo inategemea walimu kujiunga kwa wingi na kupata huduma kupitia banki hiyo.
Hamisi Milowe, Afisa elimu Msingi mwisho alisisitiza kuwa wiki ijayo tutakua na mitihani ya darasa la saba tarehe 5-6 oktoba hivyo kila mmoja kwa nafasi yake tuisimamie kwa Uadilifu kwani tuna dhamana kubwa,Matokeo yoyote yanayokuja baada ya mitihani sisi ndio wakunyoshewa vidole hvyo tujitahidi katika majukumu yetu kufundisha vizuri ili matokeo kwa Watoto wetu yawe mazuri.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.