- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
*WALIMU WA HISABATI SHULE ZA MSINGI MANYONI WAPEWA MAFUNZO KUINUA UFAULU*
*Manyoni, 19 Septemba 2025*
Mradi wa Serikali wa Shule Bora unaofadhiliwa na UKAID wenye lengo la kukuza na kuboresha Ufundishaji na ujifunzaji umeendesha mafunzo ya siku tatu kwa Walimu wa somo la Hisabati kutoka shule za msingi zote ndani ya halmashauri ya Manyoni, kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo hilo muhimu.
Mafunzo hayo yalianza tarehe 17 na kukamilika leo tarehe 19 Septemba 2025, yakifanyika katika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni yakihusisha wakufunzi wenye uzoefu kutoka Idara ya elimu Mkoa,Wilaya pamoja Wasimamizi wa Mradi huu kutoka Shirika linalofadhili mradi.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mary Kanumba Kaimu Mkurugenzi Halmashauri wilaya ya Manyoni alieleza kuwa Hisabati ni somo la msingi katika maendeleo ya kielimu, lakini limekuwa likiwa changamoto kwa baadhi ya wanafunzi. Hivyo, kupitia mafunzo haya, walimu watapewa mbinu shirikishi, rahisi na bunifu zitakazowasaidia wanafunzi kuelewa kwa urahisi.
*"Tunatarajia kila mwalimu atakaporudi katika shule yake, atakuwa na mkakati mahsusi wa kuongeza ufaulu katika somo la Hisabati. Hatutarajii kuona wanafunzi wanaogopa au kushindwa somo hili tena,"* alisema Mary Kanumba
Walimu walioshiriki walisema watajifunza mbinu mpya za kufundisha dhana ngumu za Hisabati, kutumia vifaa saidizi, pamoja na namna ya kufanya tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja.
Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa Halmashauri ya Manyoni kuinua kiwango cha ufaulu wa masomo ya msingi, hasa Hisabati, kama msingi wa mafanikio ya elimu ya juu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.