- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Afisa Tarafa ya Kintinku Ndg. Charles E. Magesa amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota katika Hafla fupi ya kuwapa Motisha Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Kata ya Chikuyu Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Hafla hii fupi imeandaliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata Chikuyu ikiongozwa na Mhe Diwani wa Kata Mhe. Benjamini Kamoga Tarehe 11 machi 2023 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Chikuyu na imewapa Motisha walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika kata hiyo lengo ni kuwafanya waongeze juhudi zaidi katika ufundishaji.
Kata ya Chikuyu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarafa ya kintinku Sekondari imekua ikifanya vizuri katika Sekta ya Elimu kwa Shule zote za Msingi na Sekondari tangu 2017 mpaka mwaka jana 2022 hivyo kamati ya Maendeleo ya kata ilikaa na kuona ni vema tukawapa motisha walimu wetu ili kuwatia moyo na kuwafanya waongeze juhudi zaidi katika ufundishaji ili kuboresha Elimu zaidi.
Akizungumza kwenye Hafla hiyo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Afisa Tarafa ya Kintinku Ndg. Charles E. Magesa amesema Tumeona juhudi za walimu wa Shule hizi za hapa Chikuyu kiukweli wanafanya vizuri sana na wana haki ya kupongezwa ili kuwafanya wawe na moyo zaidi ya kuwafundisha wanafunzi wetu na kuhakikisha tunapandisha ufaulu zaidi na zaidi.
Ninampongeza Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuhakikisha anaboresha Miundombinu ya huduma mbalimbali za jamii kama Elimu , Afya , Barabara na zingiine zote hali inayopelekea maendeleo makubwa kuonekana kwenye Nchi hii, Pia Niwapongeze sana Mheshimiwa Diwani Kata ya Chikuyu na Kamati yake ya maendeleo ya kata kwa kusimamia shuguli mbalimbali za maendeleo ya kata hii hasa miradi ambayo Mhe. Raisi wetu anaileta katika maeneo yetu, vile vile niwapongeze kwa kuona jambo hili nzuri ambalo litasaidia kuwafanya walimu kuona kuwa tunatambua juhudi zao katika kuleta maendeleo kwenye sekta ya Elimu.Niwaombe hichi mlichoanzisha kiendelee kila mwaka na isiwe hapa tuu nitaomba kata zote ziwe na mfumoo huu mzuri wa kutoa motisha kwa Walimu ili kukuza elimu katika Wilaya yetu.
Naye Ndg. Stansilaus Mongela Akimuwakilisha Afisa Elimu Sekondari amesema Moja ya mkombozi mkuu katika jamii yetu ni elimu hivyo jambo hili ni jema maana ni jitihada za kuhakikisha tunakomboa jamii yetu kwa kuwafanya walimu kuongeza juhudi katika ufundishaji. Walimu wetu wanajitoa sana kwa kufundisha vizuri hivyo jamii ninawaomba sana kuwapa ushirikiano kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanaokua wamechaguliwa kujiunga na masomo au wanaopaswa kuandikishwa shule wanaandikishwa na wanafika shule bila kukosa.,
Pia niwaombe sana kwakua mazingira yetu ya shule na jamii kuna umbali kwa wanafunzi wengine basi tujitahidi shule zetu hizi watoto wapate chakula cha mchana shuleni ili kuwapa watoto muda mzuri wa kusoma nah ii itasaidia sana watoto kujikita kwenye masomo tuu na sio kuwaza nyumbani wanapokua wanaumwa njaa, kwa hili niwaombe sana. Kwa kufanya hivi basi wanafunzi wetu watamshika sana Elimu na tutaona matokeo yake. Alisisitiza Ndg. Mongela.
Muheshimiwa Diwani Kata ya Chikuyu Mhe. Benjamini Kamoga Alisema Nawashukuru sana wageni kwa kuhudhuria hafla hii, Namshukuru Mkuu wa Wilaya kwakua alikubali kuwa Mgeni Rasmi ila kwakua ana majukumu mengine ametuma muwakilishi wake hivyo tunakukaribisha sana. Mimi na Kamati yangu ya maendeleo ya Kata tumeona vyema kuandaa hafla hii fupi ya kuwapongeza walimu na kuwapatia zawadi walilmu wote ili waendelee kufanya vizuri zaidi. Tunaahidi kuendelea kufanya hivi kwakua tunatambua mchango mkubwa wa walimu wa Shule zote zilizopo katika Kata ya Chikuyu.
Rai yangu kwa wananchi wetu na jamii kwa ujumla ni kutoa ushirikiano kwa walimu wetu na kamati za shule ili kuhakikisha tunanafanya vizuri kuhakikisha tunawatengenezea wanafunzi na walimu mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia ili kuleta matokeo chanya zaidi katika sekta ya Elimu. Alisisitiza Mhe. Kamoga.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.