- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa amewataka wananchi wa Wilaya ya Manyoni kuacha kufanya shughuli zao mbalimbali kama kilimo na kuchunga kwenye maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji kwani wanaharibu rasilimali Maji. Haya ameyasema tarehe 30 Disemba alipokua akifungua Mkutano Mkuu wa pamoja wa wadau wa maji Wilayani Manyoni uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“RUWASA wanajitahidi kuhakikisha wananchi vijijini wanapata maji kila sehemu lakini tatizo wananchi wenyewe wanakua chanzo kikubwa cha kuharibu vyanzo vya maji kwa kulima mazao yao pembeni ya vyanzo vya maji, kukata miti ovyo na kuchunga pembeni ya vyanzo na shughuli zinginezo”.
Kupitia Mkutano huu nitoe wito kwa wananchi kuacha kufanya shughuli zozote karibu na vyanzo vya maji zinazoharibu vyanzo hivi na atakaebainika anafanya hivyo jumuiya za maji naomba nipate taarifa na hatua stahiki zichukuliwe kwa uharibifu huo.Tutunze vyanzo vya maji ni muhimu sana ili viendelee kudumu na vitumike vizazi na vizazi. Amesisitiza Mhe. Mwagisa.
Nampongeza na Kumshukuru Mhe. Raisi wa awamu ya sita Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa jitihada zake za kuhakikisha wanachi wa taifa hili hasa Wilaya ya Manyoni wanapata huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maji, umeme, barabara na zingine kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya huduma hizo. Nawapongeza pia RUWASA NA MAUWASA kwa kuendelea kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi katika vijiji vyote na maeneo yote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni. Amesema Mhe. Mwagisa.
Nae Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya manyoni Ndg. Fadhili Chimsala amesema; “Kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni nawapongeza sana RUWASA na jumuiya za maji kwa kuendelea kutunza na kuendesha rasilimali hizi za maji, Maji ni rasilimali muhimu sana katika Maisha ya binadamu na maji ndio uhai hivyo tutunze rasilimali hizi vizuri ili zidumu na kutupatia maji wakati wote. Pia Maji ni rasilimali ya wote hivyo sisi kama jumuiya tunasisimamia na tuzisimamie vizuri ili watu wote wazitumie vizuri.
Afisa wa TAKUKURU Wilson Ntiro amesema Takukuru ni chombo kinachosimamia Utawala bora, kutoa elimu, kutafiti na kudhibiti Miradi ya maendeleo. Kwa nafasi zetu tunapaswa kujua tunatekeleza majukumu yetu kwa Mujibu wa sheria na taratibu za nchi hii na nia na dhamuni ni kuunga mkono juhudi na kauli mbiu ya Mhe. Dkt Samia Suluhu hassani ya kumtua mama ndoo kichwani. Hivyo kama Ofisi tutahakikisha tunaendelea kufatilia miradi ya maji kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati lakini ikiwa na kiwango cha thamani ya fedha zilizotumika.
Kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji ni kosa la jinai na ni uhujumu uchumi huo hivyo niwaombe kupitia kikao hiki na kwakua Magavana wapo hapa waambieni wananchi watunze vyanzo vya maji ili vidumu na viendelee kutupatia maji kwa matumizi yetu ya kila siku ,watakaoharibu vyanzo basi hatutosita kuchukua hatua kali dhidi yao. Amesisitiza Ntiro.
Ndg. Ntiro alisema Jumuiya hakikisheni watu au taasisi zinaouza maji zina vibali maalumu vya kufanya hivyo kwani sheria ya Maji 2009 inasema haruhusiwi mtu yeyote kuuza maji isipokua wenye kibali maalumu hivyo kwa wanaouza maji huko vijijini bila kuwa na kibali maalumu ni wanafanya kinyume cha sheria. Sio kila maji yanafaa kwa matumizi ya binadamu hivyo wataalaamu wetu Ruwasa wamepewa mamlaka ya kuyapima na kujiridhisha kuwa maji ni salama kwa matumizi ya binadamu.
Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji na Matengenezo-RUWASA Eng. Maduhu Shija amesema “ Tuendelee Kushirikiana na Jumuiya zetu ili kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma za maji safi na salama wakati wote. RUWASA tunahusika pia na Usafi wa Mazingira japo bajeti yake bado inaingia idara ya afya lakini tunapaswa kusimamia utunzaji wa mazingira.
Tuapande Miti kuzunguka vyanzo vyetu vya maji ili viendelee kuwa hali nakutupatia maji wakati wote lakini pia vitakua na mandhari nzuri sana ya kupendeza. Kwenye hili naomba nipate taarifa ya kila chanzo cha maji mmepanda miti mingapi na pia hakikisheni jumuiya zote mnawasilisha taarifa za kila mwezi kwani kwa kutokufanya hivyo tunaweza kuichukulia hatua jumuiya hiyo kwa kuifuta.Amesisitiza Eng. Maduhu
.
Mkuu wa Kitengo cha Jumuiya za Huduma za Maji ngazi ya jamii (CBWSO) Ndg Binto Manyama nae amesema; Kuanzia tarehe 16 machi 2023 tutakua na wiki ya maji mpaka tarehe 22 machi 2023 ndio siku ya kilele hivyo jumuiya zote naomba muandae mapendekezo ya mnataka kuafanya nini kwenye wiki hiyo ya maji na mapendekezo hayo niyapate ifikapo tarehe 15 januari 2023.
Pia kwa sasa tuna Jumuiya nyingi sana tuko kwenye mchakato wa kuziungnisha jumuiya hizi ili tuapate jumuiya tano hii itaongeza ufanisi wa kazi na kupunguza uwepo wa jumuiya nyingi sana.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.