- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa amewaasa watumishi kujiunga na Jeshi la Akiba ili kujenga ukakamavu wa mwili na akili lakini pia kujifunza kuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Mh Mwagisa ameyasema haya Tarehe 25 Novemba 2022 alipokua akifunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyokua yakifanyika katika kijiji cha Kamenyanga kata ya Agondi Wilaya ya Manyoni ambapo Askari wa Jeshi la Akiba wapatao 143 wamehitimu Mafunzo hayo.
Mh Mwagisa alisema "Wananchi ninawaomba sana zinapotokea fursa hizi za kujiunga na mafunzo haya ya jeshi la akiba tuendelee kujitokeza kwa wingi ili kujenga taifa lenye vijana wakakamavu wa akili na mwili na kuwafanya vijana hao kuwa wazalendo kwa Taifa lao lakini pia watumishi taasisi mbalimbali pia hii ni fursa kwenu ili kujenga afya ya miili na akili zenu hivyo ninawaasa kwa wakati ujao watumishi mjiunge kwenye mafunzo haya.
Ninawapongeza vijana hawa wanaohitimu mafunzo haya siku ya leo kwa kuonesha namna wanavoithamini nchi yao kwa kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo nguvu kazi kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali zinazozunguka kambi yao ya mafunzo ya jeshi la akiba. Alisisitiza Mh Mwagisa
Mwisho Mh Mwagisa alisema; Msimu wa kilimo umeshafika hivyo wananchi tuandae mashamba kwaajili ya kilimo cha chakula lakini pia kilimo cha biashara. Wilaya ya Manyoni tuna kampeni ya kutokomeza njaa hivyo niwaombe sana wananchi kushiriki vyema kwenye kilimo kwa msimo huu ili kujikwamua na familia zetu,
Lakini pia tuna wataalamu wetu wa kilimo tuwatumie ili tulime kilimo chenye tija na tupate mazao yatakayo tutosheleza kwaajili ya jamii yetu. Niwatakie kila la kheri katika msimu huu wa kilimo na ninaamini tutavuna sana kipindi cha mavuno kitakapofika.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria mahafali hayo ya jeshi la akiba
Mh Mwagisa akikagua Gwaride
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.