- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wazazi na jamii kwa ujumla katika Halmashauri ya Wilaya Manyoni wameaswa kutambua kuwa suala Elimu siyo jukumu la Walimu na Watumishi wa Sekta ya Elimu peke yao bali ni la kila jamii Kushiriki katika kusimamia na kuboresha masuala mbalimbali ya kielimu ikiwemo kushauri namna bora za uendeshaji wa elimu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Rahabu Mwagisa alipokuwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri tarehe 27/2/2020.
Mwagisa amesema kuwa jukumu la Elimu ni la kila mmoja kwa nafasi yake kama ambavyo Walaka wa Elimu namba 6 wa mwaka 2015 unavyofafanua.
Akitoa ufafanuzi Mwagisa amesema kuwa waraka wa Elimu bila malipo una lengo la kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata Elimu. “Serikali ya awamu ya tano imepitisha walaka huu kwa lengo la kumsadia mzazi kumpunguzia majukumu ili kuweza kumpa nafasi ya kumsomesha mtoto ili kila mtoto apate elimu ili iweze kumsaidia hapo badae” Alisema Mwaigisa.
Kuhusu usimamizi wa elimu Mwagisa alisema kuwa kazi kubwa ya Serikali ni kuajiri na kulipa walimu mishahara ,kutengeneza sera na mtaala wa elimu, na kwamba walimu wana jukumu la kuwalea wanafunzi kwa kuwapa ujuzi ,maarifa kulingana na mtaala uliopo.
Mwagisa aliongeza kuwa Maafisa Elimu wanawajibu wa kusisimamia utekelezaji wa sera za elimu wakati mzazi au mlezi wa Mwanafunzi ana jukumu la kuhakikisha anampatia mwanafunzi huduma zote kama vile kumpatia daftari,sare chakula na mahitaji mengine ya kila siku.
Akitoa rai kwa jamii Mwagissa amesema kuwa jamii ihakikishe kuwa inakagua miundo mbinu yote inayozizunguka shule za wilaya ya manyoni, na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira na shule bora ,kuhakikisha miundombinu katika kila shule inaboreshwa ili kuweza kumfanya mtoto kuona maisha ya shule ni bora.
Akitaja jukumu la mwanafunzi Mwagisa amesema kuwa mwanafunzi anajukumu la kusoma kwa bidii kuheshimu sheria na taratibu za shule husika lakini piakuwa na heshima kubwa kwa kila mtu anaemzunguka na kwa walimu pia.
“kutokana na majukumu haya ndugu wajumbe na wanajamii mnaona ambavyo sasa suala la Elimu ni la kila mmoja na siyo la mtu mmoja tu hapa kila mtu anajukumu lake”amesema Mwagisa.
Mbali na Sera ya Elimu jamii imeaswa kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto kwani ili mtoto aendelee vizuri na kupata elimu na kuweza kuwa na uwezo mkubwa darasani ni lazima alindwe vema nakuepushwa katika vitendo vyovyote vinavyoweza kumpelekea kufeli,ama kukatisha ndoto zake kielimu.
Mwagisa amewataka wanajamii kupaza sauti zao kupinga vikali unyanyasaji wa watoto na hasa watoto wa kike kwani amesema kuwa watoto wakike wanakatishwa masomo kwa makusudi na kulazimishwa kuolewa ameitaka jamii ya wanamanyoni kupiga kelele juu ya vitendo vya kikatili vinayotendeka Wilayani humo.
Naye mbunge wa Manyoni Mashariki Mh. Daniel Mtuka ameiasa jamii kuonyesha ushirikiano kwa watendaji hasa walimu ikiwemo kutembelea mashuleni na kujua changamoto mbalimbali na ameliomba jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa kesi dhidi ya unyanyasaji wa Watoto hususani wanafunzi zifuatiliwe na wanaobainika na makosa mbaimbali ya unyanyasaji ikiwemo ubakaji wafikishwe mahakamani ili iwe funzo kwa wote ambao wanafanya vitendo viovu na kuwasababisha Watoto kushindwa kuendelea na masomo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.