- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imewataka Wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini kuongeza maradufu uzalishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali katika sekta hizo kwa sababu soko la uhakika la mazao hayo lipo ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati anazindua Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kimataifa Kanda ya Kati yaliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma.
Majaliwa amesema hadi kufikia mwezi wa Sita mwaka huu tayari Serikali imepata Dola bilioni 2.3 kwa kuuza mazao mbalimbali ikiwemo matunda na jamii ya kunde nje ya nchi.
Amesema kazi iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha Maafisa Ugani wanawasaidia Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kupata masoko hayo kwa urahisi kwa njia ya Kidigitali ili wananchi waweze kunufaika ipasavyo kwa kuongeza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
“Wakulima wa Mahindi msiwe na mashaka limeni mahindi ya kutosha soko lipo “Amesisitiza Majaliwa.
Waziri Mkuu pia ameeleza kuwa kwa sasa Mataifa mbalimbali yameomba kuja kununua mahindi nchini ikiwemo Kongo, Zambia na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP- hivyo ni uda sasa kwa wakulima kutumia njia za kisasa katika kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Aidha, Majaliwa amesema kuwa hadi kufikia mwezi wa Nne mwaka huu zaidi ya Tani Milioni 13 za nyama zenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 56 zimeuza kwenye Mataifa ya Komoro, Jordan, Oman, Kuwait na Saudi Arabia.
Naye, Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego, akizungumza kwenye uzinduzi wa Maonesho hayo pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuupatia Mkoa wa Singida Mabilioni ya fedha kwa ajili ya uimarishaji wa shughuli mbalimbali za kijamii, amesisitiza kuwa mkoa utaendelea kuimarisha kwa kiwango cha hali ya juu shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili wananchi wanaofanya shughuli hizo waweze kuimarika kiuchumi na kuchangia katika pato la Taifa.
Dendego amesema mkoa wa Singida kwa sasa unaendelea kufungua mashamba ya pamoja na Sekta binafsi hasa katika zao la Korosho nia ni kuona Mkulima ananufaika kwa kiasi kikubwa na kilimo hicho katika kukuza pato lake la Taifa kwa ujumla.
Aidha, Dendego ameishukuru Serikali kwa kuupatia mkoa huo miradi mikubwa ya Umwagiliaji inayogharimu zaidi ya Bilioni 54 miradi ambayo amesema inaenda kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta elfu 17 hadi kufikia hekta 21,400 sawa na asilimia 43 ya eneo lote linalofaa kwa shughuli za umwagiliaji mkoani humo.
Dendego ameiahidi Serikali Kuu kuwa yeye na Watendaji wengine wataendelea kuimarisha sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili sekta hizo ziweze kuwakwamua wananchi kiuchumi.
Kauli mbinu ya Mwaka huu ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.