- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mh. Prof Makame Mbarawa ametembelea miradi mbalimbali ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ambapo aliambatana na mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ndugu Chales Edward Fussi pamoja na Mbunge wa Manyoni Mashariki Mh. Daniel Mtuka.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Mh Waziri ni Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni ambapo pia alipata muda wa kuzungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amewataka wahandisi wote nchini kusimamia wakandarasi wanaojenga miradi ya maji kikamilifu na kwa uadilifu. Hayo aliyasema alipokuwa akikagua miradi ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ambayo kwa sasa kuna ujenzi wa mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile awamu ya kwanza ukiwa unatekelezwa.
Mradi huu wa maji wa Kintinku/Lusilile ni mradi mkubwa ambao ukikamilika utahudumia takribani wakazi 55,485 wanaoishi katika vijiji 11. Mradi huu unategemea kugharimu kiasi cha takribani Tshs. 10,171,877,293.05.
Aidha, Mhe. Waziri amemsifu sana mkandarasi anayetekeleza mradi huu M/S CMG Construction Company ambaye ameanza utekelezaji wa ujenzi na ameshawasilisha “certificate” zake lakini bado hajalipwa.
Waziri amemuagiza Mhandisi wa Wilaya kuzihakiki “certificate” hizo za malipo ya mkandarasi huyo na kuzipeleka kwenye ngazi ya mkoani ili nako zihakikiwe ili mkandarasi huyo aweze kulipwa.
“Nitamlipa mkandarasi mwezi huu wa Februari, lakini naomba kutoa angalizo mkoa mfanye uhakiki wa kina kabla ya kuzileta Wizarani na msipofanya uhakiki wa kina nitazirejesha”, alisema Waziri Mbarawa.
Naye Mbunge wa Manyoni Mhe. Daniel Mtuka alimweleza Waziri Mbarawa kuhusu uanzishwaji wa Mamlaka ya Maji Mauwa, “Manyoni Urban Water Authority” Waziri Mbarawa amesema hana pingamizi. Wapeleke majina atayapitisha ila wachagueni watu wenye uwezo na siyo mchague watu kwa sababu ya urafiki au undugu. Chagueni watu wazuri watakaoweza kuwasaidia na kufanya kazi ya kusimamia huduma za maji hapa Manyoni.
Kabla ya kumaliza ziara yake Waziri ameeleza kuchukizwa kwake na utendaji kazi mbovu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) baada ya Mhe. Mbunge wa Manyoni Bw. Daniel Mtuka kutoa malalamiko kuhusu DDCA kushindwa kukamilisha uchimbaji wa kisima katika Halmashauri ya wilaya ya manyoni. Waziri ameagiza DDCA kukamilisha kazi hizo za kuchimba visima haraka iwezekanavyo na kusisitiza wabadilike ikiwemo mtendaji mkuu kufika na kuona namna ya kasi ya Uchimbaji inavyokwenda
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.