- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe. MIBAKO MABUBU alisema; Dhumuni kuu la ziara hii ni kujifunza kilimo cha zao la korosho kutoka katika Halmashauri ya Manyoni kwani Halmashauri ya Wilaya Manyoni ni miongoni mwa Halmashauri zinazofanya vizuri kwenye kilimo cha zao la Korosho hivyo tumeona vyema kuja kuwatembelea kuona namna mnavofanya katika kilimo hiki ili nasi tujifunze kutoka kwenu na tukafanyie kazi tutakayojifunza hapa.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni Mhe. JUMANNE SHABANI MLAGAZA aliwakaribisha wageni na kuwashukuru kwa kutembelea Manyoni na kusema kuwa lengo lao la kutaka kujifunza ni zuri kwa hiyo ni vizuri wasitumie muda mwingi ukumbini badala yake wapelekwe moja kwa moja MASIGATI kwenye mashamba ya korosho ili waweze kujionea wenyewe na kujifunza.
"Karibuni sana Halmashauri ya manyoni na tunawashukuru kwakua mmeamua kufika Manyoni ili mjionee na kujifunza juu ya zao hili la korosho hivyo basi ni vema tukaelekea kwenye mashamba ya Korosho moja kwa moja yaliopo maeneo ya Masigati ili kujifunza kwa vitendo huko huko shamabni kuliko kuchukua muda mwingi hapa ukumbini".
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni kushoto na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala kulia
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Ndg. Fadhili chimsala alisema taarifa fupi ya kilimo cha korosho kwa sasa ,kuwa hekari 1250 ndo zilianza kupandwa na kwa sasa kuna jumla ya hekari 20,000 ambazo zimepandwa korosho manyoni na ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa kuna jumla ya wakulima 1,177 waliopanda korosho ambazo zipo katika hatua tofauti tofauti ya ukuaji.zao la korosho ni chanzo kizuri cha mapato katika Halmashauri yetu ya Manyoni na tunashukuru tunapata wawekezaji wengi sana ambao ndio wanalima katika mashamba yetu haya ya pamoja ya kilimo cha korosho. Na katika Halmashauri hii tuna mashamba mengine yako katika kata ya saranda, makutopora na mkwese ambayo nayo ni ya kilimo chas pamoja.
Mtaalamu kutoka katika kituo cha TARI Halmashauri ya Manyoni pia alieleza kiufupi jinsi ya kuandaa na kupanda miche/mbegu ya korosho, lakini pia alitaja baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kuathiri zao/mmea wa korosho ambazo ni: (1) PMD(ugwili unga)- ni fangasi na aina hii ya ugonjwa unashambulia maua pindi yanapoanza kujitokeza, (2)DIE BACK(kufa kinyume)- unasababishwa na mbuu, (3) Bright . Lakini pia aliendelea kwa kutoa elimu ya jinsi gani unaweza kuzuia magonjwa haya kwa kufanya yafatayo: Usafi wa shama, kupunguza matawi/majani chini ya mkorosho na kutumia madawa/viwatilifu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kushoto na Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni kulia
Mheshimiwa diwani wa Msalala Ndg MATRIDA MSOMAA amemuomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni aweze kuahazima wataalamu wa zao la korosho kutoka Manyoni pindi nao watakapoanzisha kilimo cha zao la korosho uko katika Halmashauri yao ya Msalala na Mwenyekiti ameridhia ombi hilo na kusema kuwa watapewa wataalamu pindi watakapowahitaji ili kuwasaidia katika kuandaa kilimo cha korosho katika halmashauri yao.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.