- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa ameendelea na ziara yake tarehe 08 Novemba 2022 katika kitongoji cha chang'ombe ambapo amefanya mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi hao.Furaha isio na kifani ilionekana kwa wananchi wa Chang'ombe baada ya Mh Mwagisa kufika.
Mh Rahabu Mwagisa kabla ya kusikiliza kero za wananchi alianza kwa Kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita "Tunamshukuru Mama yetu Samia Suluhu Hassani Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea fedha nyingi katika Wilaya yetu ya Manyoni kwaajili ya Miradi mbalimbali ikiwemo Barabara,Maji,Elimu,Afya,Umeme,Kilimo na sekta zingne nyingi kwakweli Mama anaupiga Mwingi.Hivyo kwa nafasi zetu pia huku chini tunatakiwa kuisimamia na kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati lakini ikiwa na kiwango kizuri kinachoendana na thamani ya fedha zilizokuja na pia tuilinde ili idumu.
Wananchi wa chang'ombe
Mh Mwagisa alisikiliza kero za Wananchi na kuzitatua papo kwa kwa papo kwakua walikuepo wakuu wa taasisi zote na wakuu wa divisheni na vitengo,Kero zilizojitokeza ni pamoja na Afya, Maji, Umeme, Wanyama pori, Ajira za SGR, na changamoto zingine nyingi ambazo zilitztuliwa hapo hapo na Mkuu wa Wilaya.
"tuboreshe Ulinzi kwenye maeneo yetu na ikumbukwe mlinzi namba moja ni sisi wenyewe,kupitia vitongoji vyetu tuunde vikundi vya ulinzi shirikishi ili maeneo yetu yalindwe wakati wote kuepuka uhalifu.Vikundi viundwe na OCD ataleta timu yake kuwapa mafunzo ya namna ya kulinda.Pia ninaamini wanaofanya uhalifu ni watoto, vijana wetu au watu wetu wa karibu na tunawafahamu naomba wananchi wa chang'ombe tuwe tunawafichua ili kukomesha uhalifu kwenye Wilaya yetu. Alisisitiza Mh Mwagisa.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.