- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota amewataka kina mama na wanachi wa manyoni kwa ujumla kuzingatia dozi za chanjo kwa watoto kama inavyokua ikielekezwa na wataalamu wa Afya kwani kutokufata dozi za chanjo kunafanya dawa hizo zisifanye kazi vizuri.
Mhe. Kemirembe ameyasema haya alipokua akizindua maadhimisho ya wiki ya chanjo kiwilaya jana tarehe 28 aprili 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya kata ya Muhalala Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“Nitoe rai kwa kinamama na wananchi wote wa Manyoni; Kuna chanjo huwa zinatolewa zaidi ya mara moja kwa maana kuwa ili dozi yake ikamilike lazima mtoto apate chanjo zaidi ya mara moja hivyo niwaombe kina mama na wananchi wa Manyoni kwa ujumla kuhakikisha watoto wanapata chanjo kikamilifu kwa kufuata na kuzingatia dozi hizi, Sio mtoto anatakiwa kupata chanjo mara nne wewe unapata ya kwanza, ya pili unaruka unampeleka ya tatu huo sio utaratibu naomba mfate dozi ya chanjo kama wataalamu wanavyowaelekeza”
Mhe. Kemirembe amesema; Tunamshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuboresha huduma ya Afya kwetu na kuhakikisha tunapata chanjo hizi bure kwa maana kuwa tayari amelipia dawa hizi za chanjo ndio maana sisi wananchi hatutoi garama yoyote ili kuhudumiwa chanjo hizi, Hivyo tuhakikishe watoto wote wenye umri stahiki wanapata chanjo hizi ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali kwani kwa watoto kuwa wazima wakati wote wazazi tunapata Muda mzuri wa kufanya shughuli za kiuchumi lakini wakiwa wagonjwa tutakosa muda wa kukuza uchumi wetu na Taifa kwa ujumla.
Nichukue fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru watoa huduma wetu wa Afya kwa jitihada zao kubwa za kuhakikisha chanjo zinawafikia popote wananchi walipo, chanjo zote za magojwa mbalimbali zinatolewa kama vile chanjo ya Rubela, Polio, surua na zinginezo lakini pia kwa kuhakikisha Afya za wananchi wa Manyoni zinakua vizuri wakati wote, Niombe sasa chanjo hizi walau zitolewe mara mbili kwa mwezi ili kuboresha na kuongeza ufanisi zaidi katika kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo katika Wilaya yetu ya Manyoni. Alisema Mhe. Kemirembe.
Pia niwashukuru wadau wa Maendeleo ya Afya hasa CHAI waliofadhili huduma za chanjo katika halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, na wadau wengine wa Afya kama JSI na Mkapa Foundationi wanaotufadhili kifedha lakini pia kitaalamu katika Mkoa wetu na kuongeza muitikio wa waanchi katiaka kupata huduma za Afya na kuimarisha jamii yetu, Aidha napenda kuwafahamisha kuwa Wataalamu wetu wamejipanga vizuri sio tuu kutoa chanjo lakini kutoa huduma zingine za Afya ikiwa pamoja na kutoa elimu ya afya juu ya umuhimu wa kumaliza chanjo, uchangiaji wa damu salama, Afya ya uzazi ,Lishe na Magonjwa yasiyoambikizwa , Magonjwa ya mlipuko na Mengineyo. Alisisitiza Mhe. Kemirembe.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.