- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mradi wa ujenzi wa kitalu nyumba ambayo ni maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya KUTOA ELIMU kwa vijana kujifunza , kupata ujuzi wa utengenezaji wa vitalu nyumba ili kuweza kuzalisha mazao bora kwa wingi zaidi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Mhandisi kutoka SOKOINE UNIVERSITY GRADUATE ENTERPRENER COOPERATIVE (SUGECO) Rose George Ng’atigwa alisema kuwa mafunzo haya yametolewa kwa vijana 20 ambapo baada ya kukamilika kwa mradi wataongeza vijana wengine 60 ili kuweza kupata mafunzo jinsi ya kulima mazao hayo.
“Baada ya haya mafunzo ni mategemeo yetu kuwa vijana hawa watakuwa walimu kwa watu wengine”alisema Ng’atigwa.
Naye Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kuona tija ya kuwasaidia vijana kuweza kupata ujuzi huo na kwamba vijana wengi sasa wataweza kujikwamua na kunufaika na mradi huu endapo watautumia kama fursa kwao.
Chimsala amesema kuwa anawaomba vijana kuweza kutumia fursa hiyo kwani imewafikia kwa wakati na kwamba tayari kitalu nyumba kipo tayari kilichobaki ni kuotesha tu mazao ambapo mafunzo yata fanyika kwa vijana kwa vitendo.Aidha ameongeza kwa kusema kuwa wahusika ni vijana wote kutoka ndani ya Wilaya ya Manyoni.
“nitoe rai kwa vijana kuweza kujitokeza kuja kujifunza kwani mradi huu nifursa kwao kwahiyo ni vyema waache kukaa vijiweni waje pindi muda utakapowadia wajitokeze kwa wingi kwani kilimo hiki ni rahsi na mafunzo haya ni bure”Alisema Chimsala.
Zoezi la ukamilishaji ujenzi wa kitalu nyumba (green house) katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakamilika kwa Asilimia 100% .
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.